MAMA mmoja mjane, Mwajuma
Hamisi Lissu (42) ameteketea kwa moto baada ya nyumba aliyokuwa amelala
eneo la Kibamba Hondogo A maarufu Miti Mirefu jijini Dar es Salaam,
kulipuliwa kwa petroli usiku wa Agosti 24, mwaka huu.
Tukio hilo la kusikitisha inadaiwa
linahusishwa na ugomvi baada ya mama huyo kuachana na ulokole na
kujiunga tena katika dini yake ya zamani ya Kiislamu.Akisimulia
mazingira ya tukio hilo, mtoto wa pili wa mama huyo ambaye hivi sasa ni
marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Charity Jikole alikuwa na haya ya
kusema:
“Mama amelipuliwa na petroli. Baada ya moto
huo kulipuka chumbani tulikuta nyavu za kwenye dirisha la chumba
alicholala zimekatwa, tunaamini mlipuaji ndiye aliyekata nyavu hizo na
kupitishia petroli.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
“Mauaji haya siyo ya bahati mbaya bali yanatokana na mkono wa mtu kwani hata moto ulipokuwa unawaka harufu ya petroli ilikuwepo eneo hilo.
“Mkasa huu unatokana na ukweli kuwa mama
yangu awali alikuwa Muislamu lakini kutokana na matatizo yake ya kiafya
alishauriwa na baadhi ya watu kujiunga na maombi katika makanisa ya
kilokole ili awe anaombewa tatizo la presha.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.Waombolezaji wakishusha mwili wa marehemu kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
“Baada ya kushauriwa aliamua kujiunga na makanisa hayo ya kilokole akiamini kuwa angeweza kupona.Waombolezaji wakishusha mwili wa marehemu kwenye gari kwa ajili ya mazishi.
“Mama alikuwa ni mjane mwenye watoto watatu
na baada ya kujiunga na walokole amekuwa akisali katika makanisa manne
tofauti.“Sisi kama familia tunawatuhumu walokole kwa sababu hata baada
ya moto huo, baadhi yao hawakuja kusaidia kuuzima wala kutoa maji.
“Kwa kweli tulishangazwa na kitendo hicho na kuwaona ni watu wabaya sana kwetu.”Hata hivyo, mtoto huyo alisema kifo cha mama yake kimekuja siku moja baada ya kufanyiwa sherehe ya kutoka katika dini ya kilokole na kurudi kwenye Uislamu.
Mchungaji aliyetajwa kwa jina la George Said ambaye anawaongoza walokole wa eneo hilo, alipohojiwa na waandishi wetu alikiri kusikia tuhuma hizo.“Hata mimi nimesikia tuhuma hizo lakini si za kweli hata kidogo na mpaka sasa sijahojiwa na mtu yeyote au hata polisi kuhusiana na tatizo hilo,” alisema mchungaji huyo.
Uwazi lilipompigia simu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP, Camillus Wambura na kumuuliza juu ya tukio hilo, alikiri kutokea na kuongeza kuwa uchunguzi unaendelea ili kubaini chanzo chake.
0 comments:
Post a Comment