MAMA SALMA KIKWETE AHUTUBIA MKUTANO WA AFYA KUHUSU SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI, MATITI NA TEZI HUKO NEW YORK

Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama  Salma Kikwete akisalimiana na Mama Penehupifo Pohamba, Mke wa Rais wa  Namibia muda mfupi kabla ya kuhudhuria mkutano Wake wa Marais na Wakuu  wa Nchi za Afrika kuhusu masuala ya saratani ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ta tezi la kiume (prostate cancer) huko New York tarehe 24.9.2014. Mkutano huo umefadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative ya nchini Nigeria.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifanya mazungumzo na Debby Rechler (wa  kwanza kulia) akifuatiwa na Yvonne Feinstein ambao ni wafanyakazi wa  Tanzania Children Fund wakati wa mkutano wa Wake wa Marais uliofanyika  huko New York nchini Marekani tarehe 24.9.2014. Aliyesimama kushoto kwa Mama Salma ni Jill Bishop, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya TET Foundation ya Marekani.

Mkewa Rais Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake wakati wa kikao cha Wake  wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika kichozungumzia masuala ya saratani  ya shingo ya kizazi, saratani ya matiti na saratani ya tezi la kiume
huko New York tarehe 24.9.2014.

 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiteta jambo na Mama Penehupifo Pohamba  mara baada ya kuhutubia mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za  Afrika uliofanyika New York tarehe 24.9.2014. Katikati ni Princess Nikky Onyeri, Mmiliki wa Taasisi ya Princess Nikky Global Initiative and  Forum of African First Ladies Against Cervical,Breast and Prostate  Cancer ya Nigeria.


 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Wake wa Marais na Wakuu wa nchi za Afrika  wakimsikiliza Mama Salma alipokuwa anahutubia mkutano huo. 


 Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Princess  Nikky Onyeri (kushoto) na Gill Bishop mara baada ya mkutano.
(PICHA NA JOHN  LUKUWI)
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment