Julius Melema kujibu mashitaka


Julius Melema kujibu mashitaka

Kiongozi wa upinzani nchini Afrika Kusini Julius Malema, anatarajiwa kufika mahakamani kujibu mashitaka ya ufisadi.
Kiongozi huyo wa zamani wa tawi la vijana wa chama tawala, ANC, Bwana Malema mwenyewe anasifika kama mwanaharakati wa kupinmga ufisadi na pia kuwatetea wengi walio masikini.
Bwana Malema mwenye umri wa miaka 33,ambae yuko nje kwa dhamana ya randi elfu 10 anakabiliwa na mashitaka manne ya Rushwa ,ufisadi ,kughushi nyaraka na kujipatia pesa kiasi cha randi million 4 kiujanja ujanja na kuzihaulisha katika shirika moja la Ratanang linalo semekana kumilikiwa na Malema mwenyewe .

Malema anayakanusha madai hayo yote na amekua akisema anafanyiwa njama na mahasimu wake kuweza kumuangusha kisiasa
Kama ilivo dasturi yake Julius Malema ataandamana na wafuasi wake kwa wingi asubuhi ya leo kufika mahakama kuu ya Polokwane jimbo anakozaliwa mwenyewe.
Jitihada zake za kutaka kesi hiyo kutupiliwa mbali, mwaka jana hazikufua dafu. Ikiwa atapatikana na hatia ya makosa yake, huenda akapoteza kiti chake bungeni.
Wakati wa kipindi cha maswali kwa Rais mnamo mwezi Agosti, Bwana Malema, alitatiza shughili hiyo kwa kumzomea Rais Jacob Zuma akimwambia alipe pesa alizopora kutoka kwa wananchi.
Alidai kuwa Zuma alitumia dola milioni 24 mali ya umma kukarabati nyumba yake ya kifahari.
Hata hivyo Malema ambaye alifurushwa kutoka kwa chama tawala mwenyewe anadaiwa dola milioni 1.6 ambazo alipaswa kulipa kama kodi kwa serikali.
Malema aliunda chama chake cha EFF baada ya kufurushwa kutoka kwa chama tawala, baada ya kutofautiana na Rais Zuma.

 Picha: Jackob Zuma-Rais wa Afrika Kusini
Tayari msemaji wa polisi wa mkoa wa Limpopo Brig Hangwani Mulaudzi amesema ulinzi utakua mkali. Barabara za mji wa Polokwane zinazoelekea kwenye korti kuu zitafungwa kuanzia saa 12 Alfajiri polisi ikipiga doria kupambana na uhalifu wowote utakaojitokeza mkiwemo eneo la Seshogo anakozaliwa Julius Malema.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment