HUKUMU YA KESI YA KUBENEA KUHUSU BUNGE MAALUM LA KATIBA‏

Wakili wa Saed Kubenea, Peter Kibatala.
Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania imetoa uamuzi wake leo kufuatia maombi ya Saed Kubenea.
Mahakama Kuu ya Tanzania iliyokaa chini ya Judges Augustine Mwarija, Aloysius Mujulizi na Dr Fauz Twaib imetoa uamuzi wake leo kufuatia maombi ya Saed Kubenea kama ifuatavyo;
1.Kuna mgongano mkubwa kati ya toleo la Kiswahili na Toleo la Kiingereza la kifungu cha 25 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.
2. Kwamba pamoja na mgongano huo, Sheria imekusudia kwamba Madaraka ya Bunge Maalum la Katiba yatatekelezwa kupitia Rasimu ya Tume ya M.y.K kama ilivyowasilishwa kwake.
3. Kwamba mamlaka ya BMK yana mipaka, na kwamba madaraka yake yanaongozwa na na kutekelezwa kupitia Rasimu. BMK linaweza kubadili na kuboresha mapendekezo yaliyomo katika Rasimu mradi tu maboresho yasiende kinyume na misingi iliyowekwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K, kama ilivyokuwa pia kwa Tume.
4.Mahakama Kuu haina Mamlaka ya kuamua ni kiwango gani BMK inaweza kuboresha Rasimu kwani hilo ni suala la kisiasa, ingawa BMK inafungwa na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K.
Tumeridhika na maeneo kadhaa, ikiwemo msisitizo wa Rasimu hasa kwa kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali alisema Rasimu ni "working document tu".
Kuna maeneo hatujaridhika ikiwamo Mahakama kusema haina mamlaka kuamua kiwango cha maboresho ya BMK vs Rasimu.
Tutatoa taarifa zaidi baada ya kujadili.
Peter Kibatala,
Wakili wa Saed Kubenea.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment