Zarinah “The Boss Lady” Tlale a.k.a mama kijacho au kama
anavyofahamika kwa kifupi Zari, amekanusha uvumi ulioenea kuwa yeye na
mme wake wa zamani ambaye ni baba wa watoto wake watatu, Ivan Ssemwanga
kwa sasa hawazungumzi kutokana na kuwa kwenye mtafaruku mkubwa.
“Nina watoto watatu wa kiume wa kwanza ana miaka 12 wa pili 10 na mwingine ana miaka 8 wako poa na nina jivunia kuwa mama.” Alisema Zari kupitia E-Newz ya EATV.
(Kuhusu baba wa wanaye watatu) “Hatuko pamoja lakini tuko poa
kwasababu kuna vitu vingine vinaendelea kati yetu wakiwemo watoto na
mambo mengine mengi kwahiyo tuko poa. Unajua jinsi watu na vyombo vya
habari wanavyochukulia ni kama tuna ugomvi na hatuzungumzi lakini sisi
tuko poa kabisa.”
Zari pia amezungumzia kuhusu uhusiano wake na Diamond kwa kusema kuwa
mapenzi yao ni ya wao wawili na sio ya watu wengine hivyo hawapendani
ili kuwafurahisha wengine.
“Tuko poa, tunapendana lakini hakuna info zaidi. Sitaki kutoa
taarifa zaidi ambayo tunaita ‘T.M.I’ (Too Much Info) Lazima huwa kuna
kuwa na mitazamo hasi na mitazamo chanya, watu wengine watasema poa
wengine watasema sio poa, lakini mwisho wa siku sio kile watu
wanachofikiria na sio kile watu wanachotaka lakini ni nini sisi
tunataka, nini kinachotupa furaha, je tunafuraha kuwa pamoja tunataka
kuwa pamoja, ndo hivyo. Hatudate kwaajili ya watu, au kwasababu wao
wanataka tuwe pamoja.”
Home / Bongo yetu /
isikupite /
Ma Star wetu /
Utaipenda
/ Zari akanusha uvumi kuwa hana maelewano na baba wa wanaye watatu
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment