Hii ni taarifa ya umma iliyotolewa na mtandao wa waandishi kupitia
mitandao nchini inayomuomba Rais Jakaya Kikwete kutoupitisha muswada wa
sheria ya makosa ya mtandaoni, 2015:
Mtandao wa waandishi kupitia mitandao nchini, Tanzania Bloggers
Network (TBN) tunamuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.
Jakaya Mrisho Kikwete kutumia mamlaka yake vyema kwa kutokupitisha
muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao, 2015 unaokandamiza uhuru wa
mawasiliano mitandaoni.
Muswada wa sheria ya makosa ya Mtandaoni unaainisha makosa
yanayohusiana na matumizi ya mfumo wa kompyuta na Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano, na kuweka utaratibu wa upelelezi, ukusanyaji na matumizi
ya ushahidi wa kieletroniki na masuala mengine yanayohusiana na hayo.
MUSWADA WA SHERIA YA MAKOSA YA MTANDAONI, 2015
Umoja huu (TBN) ulishtushwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kukubali kupitisha Muswada wa Sheria ya Makosa ya Mtandao 2015
kwa hati ya dharura kitendo ambacho hakikutarajiwa kutokana na kuwa
mitandao bado ni kitu kipya nchini hivyo tulihitaji maridhiano na wadau
na elimu kati ya raia na Serikali ili wengi watambue yapi ni makosa kwa
kutumia mitandao na yapi yanakubalika.
Kimsingi TBN haipingi Tanzania kuwa na Sheria ya Makosa ya Mtandao
bali inaiomba Serikali kuwashirikisha wananchi na hasa wadau wa habari
na wanamitandao ya jamii ili kuridhiana kwa vipengele ambavyo
vinaonekana kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari. Na hatimaye kutoka
na sheria isiyo na viashiria kandamizi juu ya uhuru wa kupata na pokea
habari.
Hali kadhalika tulishuhudia watetezi wa haki za binadamu pamoja na
wawakilishi wa watumiaji wa Mtandao wa intaneti nchini wakitoa sababu
zenye uzito za kwanini sheria hii isipite kwa hati ya dharura na kuhoji
kwanini sheria hii ipite kwa dharura bila ya kupata majibu.
Muswada huu ambao kati ya makosa mengi uliyonayo kubwa moja wapo ni
majukumu makubwa aliyopewa Mkuu wa Kituo chochote cha Polisi kuwa na
uwezo wa kupekuwa na kuchukua vielelezo/data pale anaposhuku kuna suala
la uhalifu unaohusu mtandao. Swali ni kuwa kwanini polisi apewe mamlaka
ya kumsulubisha mtuhumiwa katika hatua ya mwanzo bila uthibitisho wa
sahihi?
Mbali na hapo, sisi kama waandishi ulimwenguni kote tunatakiwa
kufuatilia maadili ya kazi zetu. Maadili ya mwandishi yeyote yule ni
kutunza usiri wa chanzo cha habari yake pale inapotakiwa lakini katika
sheria hii sisi kama bloggers, sheria hii inakiuka hili kwa
kutulazimisha kutaja vyanzo vya habari.
Kupitia sheria hii, bloga yeyote yupo hatarini kutokana na kwamba
sheria inaainisha ni kosa la jinai kutoa ujumbe unaoweza kumuudhi mtu
kihisia.
Aidha, tunamuomba Mheshimiwa Rais pia asipitishe Muswada wa Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2013.
Muswada huu unavinyima uhuru vyombo vya habari vinavyotangaza takwimu
mbalimbali. Kama ilivyo Ibara ya 7(4) ‘‘Chombo chochote cha habari
ambacho kinachapisha taarifa za kitakwimu za uongo au upotoshaji, au
kinatangaza kipindi chochote kinachohusu shughuli za ukusanywaji wa
taarifa ambayo imefanywa au inafanywa na Ofisi, na hatimaye kusababisha
wananchi wasishiriki kwenye shughuli hiyo ya ukusanywaji wa taarifa au
wasishirikiane na maafisa wa Ofisi, kinatenda kosa.’’
Hii iki maanisha kuwa hata blog zetu ziko hatarini kuelekea katika
kulazimika kufanya kazi za kuisifia serikali na kutangaza takwimu
zilizopitiwa na serikali tu, jambo ambalo litaharibu ukuaji wa uhuru wa
habari nchini.
Tunamkumbusha mwananchi wa kawaida anayetumia mtandao wa intaneti
kuwa hayuko salama kwani sheria hii inamlazimisha mtoa huduma wa mtandao
kutoa taarifa za wateja wake jambo ambalo linahatarisha uhuru wa kutoa
na kupokea habari.
Chanzo Bongo 5
Home / Bongo yetu /
isikupite /
News /
Science & Technology /
Utaipenda
/ Rais Kikwete aombwa kutoupitisha muswada wa sheria ya makosa ya mtandaoni, 2015
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment