Jeshi
la Magereza nchini limemfukuza kazi askari wake wa Gereza Bariadi,
Mkoani Shinyanga (pichani) kwa kosa la kupatikana na fadha za bandia
kinyume na Sheria za Nchi.
Kwa
mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa jana Machi 28, 2015 na kusainiwa na
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja, askari Na. B.
6499 Wdr. Edmund Masaga amefukuzwa kazi kwa fedheha kuanzia Machi 28,
2015 kwa kosa la kulidhalilisha Jeshi mbele ya Umma kinyume na Kanuni
22(xlix) ya Kanuni za Utumishi wa Jeshi la Magereza za Mwaka 1997.
Aidha,
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amekemea vikali
vitendo hivyo kwani ni kinyume cha Maadili na Utendaji ndani ya Jeshi
la Magereza huku akiwataka askari wote wa Jeshi la Magereza nchini
kutenda kazi zao kwa uadilifu na uaminifu mkubwa.
Imetolewa na; Lucas Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
Afisa Habari wa Jeshi la Magereza,
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
Machi 29, 2015.
0 comments:
Post a Comment