Muongozaji wa video Adam “AJ” Juma wa Visual Lab/Next Level, amesema
kuwa vita katika sanaa baina ya waongozaji wa video na watayarishaji wa
muziki huleta chuki na kuididimiza sanaa nzima.
“Hizi vita za katika sanaa za kijinga sana, hazileti maendeleo bali
chuki tu. Vita kati ya madirector sio jambo lakushangilia hata kidogo,
kwani mtu ukiwa wa kwanza wa pili maana yake nini? Mnapoteza urafiki kwa
ummaarufu wa siku mbili. Kitu hiki kilifanyika kwa pfunk na mj, then
dunga na mapigo then lamar, wako wapi hawa watu ambao ndio mngongo wa
mziki. Ukiwaangalia hawa maproducer wote ni wakali ila ujinga ndio
umesabisha ubishani usiokua na maendeleo. Tujifunze kupenda na kuangalia
style za wenzetu sio kwa lengo lakusema nani ni mkali au nani ni
wakwanza, kwa nia hiyo tutakuza sanaa. Sijawahi hata siku moja kufikiria
kwamba nimfunike mtu flani au niwe on top, bali nafanya kwa kadri ya
uwezo wangu kuwa tafauti mengine nawaachia watazamaji. Sitaki
kufananishwa na mtu yoyote yule kwa uzuri wala ubaya, kama hujaelewa
nachokifanya nunua camera fanya wewe. Nawaonya nyie mnaogombana mkiwa
mmesahau mlipotoka, UMOJA NI NGUVU UTENGANO NI UDHAIFU. Hakuna aliyebora
kati yetu wote tunaudhaifu wetu.”
ADAM JUMA: "CHUKI BAINA YETU ZINATURUDISHA NYUMA SI WASANII, PRODUCER NA HATA MA DIRECTOR"
28 March
Bongo yetu
,
Ma Star wetu
,
movies
,
News
0 comments:
Post a Comment