KISIGA ATUA SIMBA



  Kiungo wa Simba Shabani Kisiga.



KIUNGO wa Simba ambaye alijiondoa kwenye kikosi hicho kwa madai ya kutoridhishwa na baadhi ya mambo ya ndani ya klabu hiyo, Shabani Kisiga jana jioni alitinga kwenye mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Dege Beach, Mbweni jijini Dar.

REPOTER wetu alimshuhudia Kisiga aliyekuwa amevalia mavazi ya kiraia akitinga mazoezini hapo na baadaye akaungumza na kocha wa kikosi hicho, Goran Kopunovic kwa zaidi ya dakika tano kabla ya kumuacha nje ya uwanja na kwenda kuendelea na program ya kuwanoa vijana wake.

Hata hivyo baada ya mazoezi kumalizika kocha huyo alirejea na kuungana na kocha msaidizi, Selemani Matola na kiongozi wa Simba, Salim Swaka ambapo walionekana wakizungumza na kiungo huyo lakini inaonekana hawakufikia muafaka kwani baada ya kumaliza viongozi hao waliondoka pamoja tofauti na Kisiga ambaye alitimka kivyake.
tulijaribu kuwahoji wahusika hao kwa nyakati tofauti mazoezini hapo kuhusiana na kile walichokuwa wakikizungumza na Kisiga ambapo wote waligoma kuliongelea suala walilokuwa wakilijadili.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment