
Kwa mujibu wa Idris, nyumba hiyo ipo maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar hivyo kwa sasa naye ni baba mwenye nyumba.Mjengo wa ghorofa uliononuliwa na mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan.Jamaa huyo alitarajia kuhamia kwenye mjengo huo jana Jumapili.
Takribani wiki saba tangu anyakue zaidi ya Sh. Milioni 500 baada ya kuibuka mshindi kwenye Shindano la Big Brother Africa ‘Hotshots’ 2014, Idris Sultan anadaiwa kubakiza takribani kiasi cha Sh. milioni 200 baada ya kudaiwa kununua mjengo wa ghorofa wenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 300.

Wataalam hao walifafanua kwamba, Idris anatakiwa kuzitumia fedha hizo kujiongezea kipato la sivyo atazitumia kuhudumia nyumba hiyo kwa vitu kama kulipia bili mbalimbali, kodi na kuajiri wahudumu.
“Anaweza akaona kwamba kununua nyumba ni matumizi mazuri ya fedha alizoshinda lakini anatakiwa awe makini, aidha kwa kufanyia biashara au kutoa huduma itakayokuwa ikimwingiza kipato.
“Pia asisikilize watu wanasema nini juu ya fedha zake. Anatakiwa kutimiza ndoto zake alizokuwa nazo kabla hajazipata,” alisema mmoja wa wataalam hao ambaye hakupenda jina lake liandikwe.
0 comments:
Post a Comment