DAVINA ASIMULIA ALIVYO PATA MATESO JELA


NGULI wa filamu za Kibongo, Davina Yahaya ‘Davina’, amesema kamwe hatokuja kusahau mateso aliyowahi kuyapata akiwa Gereza la Segerea ambapo alikaa kwa siku tatu.
Nguli wa filamu za Kibongo, Davina Yahaya ‘Davina’.
 Davina alisema tukio hilo lilitokea mwishoni mwa mwaka 2012 ambapo ilikuwa ni tatizo la kifamilia lililosababisha kutupiwa huko japokuwa hakuweza kuliweka hadharani kwakuwa bado lipo mikononi mwa sheria.
“Huwa natokwa machozi na kamwe sitokuja kusahau mateso niliyoyapata Segerea. Nilikuwa kwa siku tatu lakini niliona kama mwezi, hali ya hewa, sehemu ya kulala zilikuwa mbaya sana, wingi wa watu na sikupata hata nafasi ya kulala zaidi ya kukesha nikilia,” alisema Davina.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment