AZAM , YANGA ZASHARE KITI KIMOJA HUKU AZM IKIWA JUU KWA MAGOLI



TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi mnono wa mabao matano 'mkono' dhidi ya mawili yaliyofungwa na Mtibwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara iliyopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam jioni hii.
Mabao ya Azam yamefungwa na Didier Kavumbagu aliyetupia mawili pamoja na Frank Domayo ambaye naye amefunga mawili huku bao la mwisho likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.
Mabao mawili ya Mtibwa Sugar yamefungwa na Musa Nampaka na Ameir Ally.
Kwa matokeo ya leo, Azam wamerudi tena kileleni wakiwa na jumla ya pointi 25 sawa na Yanga lakini wakiwazidi Yanga kwa tofauti ya mabao.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment