Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete
akipokewa na Dkt. Peter Feiler, Mkuu wa Idara ya Ushirikiano wa
Kiuchumi katika Wizara ya Ushirikiano wa Kiuchumi na Maendeleo ya
Ujerumani wakati alipowasili kwenye Ofisi ya Ubalozi wa Ujerumani kwenye
Umoja wa Mataifa huko New York alipokwenda kuhudhuria mkutano
uliozungumzia masuala ya elimu: kuwawezesha vijana kufanya maamuzi
sahihi ya kiafya tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi
na Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (kulia) na Mke wa
Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika wakati wa ufunguzi wa
mkutano ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani kuzungumzia masuala ya
elimu ili kuwawezesha vijana barani Afrika kufanya maamuzi sahihi ya
kiafya.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akisalimiana na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na Maendeleo wa
Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller wakati wa mkutano wa kuzungumzia
masuala ya elimu kwa ajili ya kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahihi
ya kiafya barani Afrika.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akipiga picha ya pamoja na Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi na
Maendeleo wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller (wa pili kulia) na Mke wa
Rais wa Malawi Mheshimiwa Getrude Mutharika (wa pili kushoto).
Aliyesimama wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako Manongi na wa kwanza kushoto ni Msaidizi wa Mke wa Rais wa Malawi.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Mke wa Rais wa Malawi Mheshimiwa
Getrude Mutharika wakati wa mkutano wa kujadili masuala ya masuala ya
elimu ili kuwawezesha kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo ni
sehemu ya Maandalizi ya Mkutano wa Mwaka wa Marais na Wakuu wa Nchi za
Umoja wa Mataifa.
Baadhi ya washiriki
kwenye mkutano uliojadili masuala ya elimu kwa vijana wa Afrika ili
wafanye maamuzi sahihi ya kiafya wakisikiliza hotuba ya Mama Salma
Kikwete.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akihutubia mkutano wa masuala ya elimu kwa vijana wa bara la
Afrika ili waweze kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Mkutano huo
umeandaliwa na serikali ya Ujerumani na ulifanyika huko New York tarehe 22.9.2014.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akiwa na wageni wengine mashuhuri wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano wa kujadili masuala
ya elimu kwa vijana wa Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya
ulioandaliwa na serikali ya Ujerumani. Aliyekaa wa kwanza kushoto ni
Waziri wa Ushirikiano wa Uchumi wa Ujerumani Mheshimiwa Gerd Mueller
akifuatiwa na Mama Getrude Mutharika na wa kwanza kulia ni Mjumbe Maalum
wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Masuala ya Vijana Bwana Ahmed
Alhendawi.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akibadilishana mawazo na Mke wa Rais Malawi Mama Getrude
Mutharika mwishoni mwa mkutano wa kujadili masuala ya elimu kwa vijana
barani Afrika kuhusu kufanya maamuzi sahihi ya kiafya. Aliyesimama
katikati ni Balozi wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa Ndugu Tuvako
Manongi.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akibadilishana mawazo na Dkt. Sheila Tlou, Mkurugenzi wa UNAIDS – Regional Support Team
for Eastern and Southern Africa na Waziri Mstaafu wa Afya wa Botswana
na kushoto ni Mke wa Rais wa Malawi Mama Getrude Mutharika mara baada ya kumalizika mkutano wa siku moja uliofanyika huko New York
0 comments:
Post a Comment