MARCOS ROJO RASMI MAN UTD, APEWA JEZI NAMBA 5


KLABU ya Manchester United imekamilisha usajili wa beki wa Sporting Lisbon, Marcos Rojo aliyesaini mkataba wa miaka mitano kuichezea klabu hiyo.

Marcos Rojo akiwa na jezi yake namba 5.
Marcos Rojo ametua klabuni hapo kwa ada ya pauni milioni 16 baada ya makubaliano na timu yake ya zamani ya Sporting Lisbon iliyomchukua kiungo wa Man United Luis Nani kwa mkopo.
Rojo akitoka hotelini jijini Manchester United.
Akiwa Sporting Lisbon, Nani ataendelea kulipwa mshahara wake wote na klabu yake ya Manchester United aliyoitumikia kwa miaka saba akitokea timu hiyo aliyokwenda kwa mkopo.
Rojo anakuwa mchezaji wa tatu kusajiliwa na United kwa msimu huu baada ya usajili wa Luke Shaw na Ander Herrera.

Marcos Rojo ndani ya Manchester United.
Beki huyo anayeichezea timu ya Taifa ya Argentina atavaa jezi namba 5 aliyokuwa akivaa beki Rio Ferdinand.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment