ESHA BUHETI GONJWA GONJWA, TUMUOMBEENI


MUIGIZAJI aliyelamba tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike katika Tamasha la Zanzibar Festival Film ‘ZIFF’ mwaka huu, Esha Salim Buheti hali yake siyo nzuri na anahitaji maombi ili apone kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi.
Mwigizaji, Esha Salim Buheti akiwa hoi kitandani.
Akizungumza na Ijumaa lililokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Esha alisema, alifikishwa hospitalini hapo juzi Jumatano akiwa na hali mbaya kufuatia ‘kuendesha’ ile mbaya.
“Nilifikishwa hapa nikiwa na hali mbaya, nilikuwa ‘naendesha’ sana hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu, ilibidi wanichukue vipimo ili kujua tatizo.
Akihudumiwa Hospitalini.
“Baadaye wakaniambia nina uvimbe kwenye kizazi na UTI, yaani dah! Naomba Mungu anisaidie na naomba mashabiki wangu pia waniombee nipone,” alisema Esha.
Share on Google Plus

About ahmed

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment