
Belle 9 ana kila sababu ya kufurahia mafanikio mapya, kwasababu kwa mara ya kwanza video yake ya ‘Shauri Zao’ iliyotoka kwenye vituo vya nyumbani wiki kadhaa zilizopita, imetambulishwa na kituo cha Ufaransa, Trace Urban na kuwa ndio video yake ya kwanza kuchezwa na kituo hicho cha kimataifa.
Belle kupitia Instagram ameshare screenshots na kuandika;
“Much respect and big time appreciation for ur support , our utmost gratitude goes out to the whole trace network @trace_urban @tracenigeria”
Video ya ‘Shauri zao’ imeongozwa na Hanscana na imefanyika hapa hapa Tanzania, hii ikiwa ni ishara kuwa kama msanii akiwekeza na kazi ikasimamiwa vizuri kuna uwezekano video za watayarishaji wa nyumbani zikaeleweka kwenye vituo vingi vya kimataifa.
0 comments:
Post a Comment