
Mwanamuziki wa kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka kuja
na kampeni ya ‘Uchaguzi kwa Amani’ ili kuweza kuwahamasisha vijana
kushiriki uchaguzi mkuu kwa amani.
Nikki wa Pili amesema kuwa wazo hilo limemjia baada ya kuona tangu
mwaka 1995 vurugu zimechukuliwa kama sehemu ya kampeni hivyo kampeni
hiyo itasaidia kuwahamasihsa watanzaniakushiriki uchaguzi wa 2015 kwa
amani.

Msanii huyo kutoka mkoani Arusha ameongeza kuwa walengwa wakubwa wa kampeni hiyo watakuwa ni vijana kwahiyo wataanza kuongea na vijana wenzao kuwa demokrasia ni malumbano ya hoja, siyo malumbano ya vikundi, kwa hiyo wasimtazame mtu na chama chake, bendera yake, na kuongeza kuwa mtu atazamwe kwa hoja na ajibiwe kwa hoja.

0 comments:
Post a Comment