
Awali ni Rostam Aziz ndiye aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo.
Kwa mujibu wa Forbes, Dewji mwenye umri wa miaka 39 ana utajiri wa dola bilioni 1.3. Utajiri huo unamfanya mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mbunge wa Singida Mjini, kushika nafasi ya 1,500 katika orodha ya watu matajiri duniani, nafasi ya 31 barani Afrika na nafasi ya kwanza Tanzania.
Rostam Aziz, 50, mwenye utajiri wa dola bilioni 1 anakamata nafasi ya 1,741 duniani, nafasi ya 32 barani Afrika na nafasi ya pili nchini.
0 comments:
Post a Comment