
Akiongea na E-News ya EATV, Izzo alisema:
Hii inakuwa rekodi ya kwanza kwangu kusimamiwa chorus na nyota wa kike ambaye ni Shaa. Halafu unajua jina la Kidawa ni majina ya watoto wa kike ambao wamezoeleka huko uswahilini. Huwezi kukuta mtoto anaitwa jina hilo Masaki, Mikocheni,Oysterbay. Sasa humu nimeelezea kuwa hili jina la Kidawa unaweza kulinyambulisha tofauti na watu walivyozoea. Hii unaweza kumueleza hata mtu wako wa karibu kupitia jina la Kidawa. Kwahiyo mashabiki wakae tayari kusikia hiyo ngoma.”
Hivi karibuni kupitia Instagram, Izzo aliandika: Naomba mnisikilize vizuri na Naomba mninukuu hii kauli yangu “Baada ya video hii ya KIDAWA kutoka Asilimia 98% ya wanawake waliopo kwenye Mahusiano(mapenzi) watabadili majina yao na kujiita wakina KIDAWA au a.k.a zao zitakuwa KIDAWA…..Fanya kumtag yoyote ambaye yupo kwenye mahusiano ajionee ili. KIDAWA VIDEO COMING SOON.
0 comments:
Post a Comment