




Kundi la ”Wakali Sisi” lenye makazi yake Kiwalani jijini Dar es Salaam, ambalo liliibuka na ushindi miongoni mwa makundi matano yaliyoingia fainali za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% na kujishindia kitita cha shilingi milioni 5 wiki iliyopita leo/ jana wasanii wa kikundi hicho walikabidhiwa simu aina ya smart Phone na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom.
Akiongea katika hafla ya kuwakabidhi zawadi ya simu Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alisema kuwa kwa kushinda mashindano hayo wamedhihirisha kuwa wana kipaji kikubwa na aliwataka wasibweteke bali wajiendeleze ili waweze kupata mafanikio zaidi.
“Vodacom tunaamini kuwa sanaa na michezo inaweza kutoa ajira kwa vijana ndio maana tumekuwa tukidhamini michezo na sanaa hivyo tumia vizuri pesa mlizopata na simu hizi tulizowazawadia kutafuta fursa za kusonga mbele na kupata mafanikio zaidi nasi tutazidi kuwaunga mkono”Alisema Nkurlu.
Naye msemaji wa kundi hilo Baraka Kambona aliishukuru kampuni hiyo kwa zawadi hizo za simu na kuongeza kuwa mashindano hayo yamewafumbua macho na wameweza kujulikana na kuahidi kuendelea na mazoezi na ubunifu zaidi ili kundi lao lizidi kutamba katika ushindani mkubwa wa sanaa ya muziki kwani hata jana tulitumbuiza kwenye shindano la Miss Tanzania.
Shindano hilo linaloratibiwa na Kituo cha East Africa Television na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, lilikuwa la kukata na shoka kwa ushindani mkali na lilifikia tamati Oktoba nne katika Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Makundi matatu yalifanikiwa kujinyakulia zawadi mbalimbali katika hatua ya fainali hiyo na vijana walikuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wakali sisi walioibuka kidedea na kujinyakulia kitita cha Sh5 Milioni huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone Smart Kick ikiwa na muda wa maongezi wa Sh 100,000.
Mshindi wa pili ni kundi la The W.T. ambalo lilijinyakulia Sh1.5 Milioni na mshindi wa tatu ni kundi la Wazawa Crew lilijinyakulia Sh500,000.
0 comments:
Post a Comment